
Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Hiiti Silo (kushoto) akionyesha namna wajasiriamali wanavyoweza kuzingatia suala la usalama kwenye bidhaa
Mafunzo hayo yaliyolenga kufanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam yameandaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania (TFDA) katika kutekeleza moja ya majukumu yake ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanakuwa salama pindi wanapotumia bidhaa zozote za chakula.
Akizungumza katika Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa TFDA Raymond Wigenge amesema lengo ni kuhakikisha bidhaa wanazozalisha zinakuwa na zinakuwa na viwango stahiki.