
Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Profesa Githu Muigai
Majaji saba GBM Kariuki, Milton Makhandia, William Ouko,Kathurima M'ilnoti,Patrick Kiage, Jamila Mohammed, Otieno Odek, walielezwa kuwa madai kwamba Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Profesa Githu Muigai alikutana na mmoja na wajumbe tume hiyo hayana msingi wowote.
Jaji Rawal alimuomba Jaji Makhandaia ajiondoe katika kesi hiyo kwa alikutana na Prof. Muigai na kuamriwa rufaa ya kupinga kustaafu kwa Naibu jaji Mkuu ifutwe.
Jaji Rawal alitakiwa kustaafu kazi January 15 mwaka huu baada ya kufikisha miaka 70 lakini amepinga na kusema kuwa anatakiwa kustaafu akiwa na umri wa miaka 74 kama alivyoambiwa alipoteuliwa chini ya katiba ya Zamani.
Jaji Philip Tunoi wa Mahakama ya juu pia amemtaka Jaji Kariuki ajiondoe katika rufaa yake ya kupinga kustaafishwa ambako Majaji hao saba watatoa uamuzi March 11 mwaka huu.