Thursday , 5th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imesema inafanya juhudi za kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya elimu, ili kukidhi mahitaji muhimu ya wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari ikiwa ni pamoja na kutatua tatizo la upungufu wa madawati.

Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Akijibu maswali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda amesema ufinyu wa bajeti katika wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kutofikiwa kwa malengo ya kupunguza changamoto hizo kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na darasa la kwanza.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Jenister Mhagama ametoa azimio kwa bunge la kutaka kukiwezesha chuo cha ustawi wa jamii Tengeru kilichopo Arusha kuwa Taasisi inayojitegemea kiutendaji ili kutoa elimu yenye hadhi za shahada na kutoa fursa ya wanafunzi wengi kupata fursa ya kujiunga na chuo hicho.