
Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu.
Siku ya kwanza ya ziara yake, Lissu atakuwa nchini Ujerumani kwa siku mbili, ambako atakutana na baadhi ya maofisa wa Serikali pamoja na wabunge wa Bunge la Ujerumani.
Baada ya hapo Lissu atazuru Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) Brussels, Ubelgiji ambako atakutana na baadhi ya watendaji wa jumuiya hiyo, wabunge wa EU pamoja na wanadiplomasia wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha nchi zao EU.
Aidha Lissu ataelekea Marekani kwa siku 10 ambapo mbali ya kukutana na watanzania wanaoishi nchini humo, atakutana na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pamoja na Watendaji wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID).
Ziara hiyo huenda ikamuingiza Mbunge wa Singida wa Mashariki Tundu Lissu kwenye vita nyingine Spika wa Bunge Job Ndugai baada ya ile ziara ya kwanza ambapo aliyozuru nchini Uingereza huku Spika Ndugai akimtaka Mbunge huyo kurudi Tanzania kwa kuwa hana kibali cha kukaa nje ya nchi.