Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwanzilishi na Mbia mwenza wa taasisi inayojishughulisha na uwekezaji kwenye sekta ya afya ya Totohealth yenye makao yake mkoani Kilimanjaro Bi. Guilia Besana, wakati akizungumzia ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma bora za afya.
Mpango wa Bi. Besana umeungwa mkono na Mwakilishi Mkazi wa mfuko wa Human Development Innovation Fund HDIF, unaohusika na ufadhili wa pesa kwa miradi ya ubunifu ambao makao yake makuu yapo nchini Uingereza Bw. David McGinty, ambaye amesema ubinifu wowote unaolenga kutoa suluhisho la matatizo katika jamii unaweza pia kuwa chanzo kizuri cha mapato na ajira kwa watu wa jamii husika.
