Monday , 5th Sep , 2016

Uchumi wa dunia unakabiliwa na kitisho kutokana na kuongezeka hali ya kila nchi kulinda soko lake na kuhatarisha uwezo wa masoko ya fedha

Rais Barack Obama (Kulia) akiwa na Rais wa China Xi Jinping.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa China Xi Jinping katika ufunguzi wa mkutano wa kilele wa siku mbili wa viongozi wa mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi duniani yajulikanayo kama G20.

Onyo la Rais huyo wa China limekuja baada ya kufanyika mkutano kati yake na Rais wa Marekani Barack Obama ambaye ameutaja kuwa wa mafanikio.

Hata hivyo kikao cha viongozi hao wawili kimeshindwa kuzileta karibu pande zote mbili katika kuyapatia ufumbuzi masuala kadhaa tete kama vile suala la mvutano katika bahari ya Kusini mwa China.

Kadhalika viongozi wa kundi hilo la G20 wanajiandaa kufikia makubaliano katika taarifa ya pamoja mwishoni mwa mkutano wa kilele, itakayojumuisha sera zote na hatua za kuchukuliwa kuhusu masuala ya kiuchumi na mageuzi ya kimuundo