
Obasanjo amesema uhuru wa kujieleza kukusanyika na kuwasilana na umma wa kila kiongozi sharti ulindwe na kama kuna vizuizi dhidi ya kiongozi yeyote lazima viondolewe.
Aidha wakati Obasanjo anayasema hayo kiongozi wa upinzani ambaye pia aligombea uchaguzi huo Dkt. Kizza Besigye bado anashikiliwa katika kizuizi cha nyumbani kwake baada ya kutaka kuitisha maandamano ya kupinga uchaguzi huo uliomrejesha madarakani Rais Yoweri Museveni.
Wakati huo huo Obasanjo ambaye aliongoza ujumbe wa Jumuiya ya Madola uliokuwa ukiangalia vigezo vya kidemokrasia katika uchaguzi uliokamilika nchini Uganda amewashauri viongozi wa uganda kujiepusha na makabiliano na migongano baina yao.
Chanzo BBC