
Hayo yamesemwa na balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose alipomtembelea Rais Dkt.Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam.
Amesema juhudi za mapambano dhidi ya ufisadi pamoja na kubana matumizi na ubadhirifu wa mali za umma kunakotekelezwa kwa vitendo na serikali ya awamu ya tano ni mfano wa kuigwa.
Aidha Balozi Melrose amesema waziri mkuu wa nchi ya Uingereza, David Cameroon amevutiwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli na kusisitiza kwamba nchi hiyo itaendeleza ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Uingereza na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo.