Rasi Magufuli akifanya mazungumzo na Guterres
Bwana Guterres ametoa hakikisho hilo wakati wa mazungumzo kati yao, kando mwa mkutano wa wakuu wa Muungano wa Afrika, AU huko Addis Ababa, Ethiopia.
Amesema Umoja wa Mataifa utatia msisitizo zaidi katika kuhimiza wadau mbalimbali wa maendeleo wa jumuiya ya kimataifa kuchangia juhudi zinazofanywa na Tanzania za kuwapatia hifadhi wakimbizi wa nchi mbalimbali tangu mwaka 1971.
Kwa upande wake Rais Magufuli ameelezea juhudi za Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki za kushughulikia mzozo wa Burundi, akisema harakati hizo zinazoongozwa na Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa zinaendelea vizuri