Monday , 9th May , 2016

Uongozi wa Soko la Buguruni jijini Dar es Salaam umesema kuwa wanaunga mkono uamuzi wa Manispaa ya Ilala kuamua kufanya usajili wa wafanyabiashara wanaofanya biashara katika soko hilo kwani utawarahisishia katika ukusanyaji wa mapato.

Akiongea na East Africa Radio Mwenyekiti wa Soko hilo Bw Saidi Habibu amesema kuwa hapo awali kulikuwa hamna takwimu sahihi za wafanyabiashara hao hali iliyopelekea ugumu katika kukusanya mapato na upatikanaji wa huduma nyingine za kijamii kama upanuzi wa soko.

Aidha, Bw Habibu amesema kuwa soko hilo linakabiliwa na ufinyu wa miundombinu hivyo halina uwezo wa kupokea wafanyabiashara wapya watakaoondolewa katika maeneo yasiyo rasmi.