Thursday , 3rd Jan , 2019

Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kuupitishwa kuwa sheria.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe.

Kesi hiyo imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari 4,2019 huku mlalamikiwa akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akisoma tamko la umoja huo leo Alhamisi Januari 03, 2019, Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema muswada huo unakinzana na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 hivyo ni muhimu kwao kuupinga.

Tunawaomba wanachama wetu wote kesho tufike kwa wingi mahakamani kusikiliza kesi hii, wanademokrasia waone kwamba hatujakaa tunachukua hatua,” amesema Zitto

Amesema muswada huo unalenga kuvikandamiza vyama vya siasa na kufanya shughuli zote za kisiasa kuwa jinai.