Sunday , 13th Jan , 2019

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla mchana huu anakutana na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, huku kila mmoja akitamba kuwa atashinda kwenye mkutano huo.

Fatma Karume kushoto na Hamis Kigwangalla kulia.

Viongozi hao wawili wanakutana katika mzungumzo ambayo yanahusisha chakula cha katikati ya asubuhi na mchana maarufu kama 'Brunch' ambayo wao wameamua kuiita 'Brunch date' huku kila mmoja akitamba ataibuka mshindi kwa kula pamoja na hoja.

Mapema leo Fatma ameanzia kwenye mazoezi huku akimtahadharisha Kigwangalla kuwa mazoezi hayo ni kwaajili yake hivyo ajipange na 'Wallet' yake vinginevyo atakosa pesa ya kulipia na ataosha vyombo'

Naye Kigwangalla amejibu kwa kumtishia Shangazi kuwa atamshinda na endapo atamletea uzungu mwingi kwasababu ni mtoto wa kishua na yeye ni mtoto wa uswahilini atatumia lugha ya Kinyamwezi kummaliza.

'Brunch date' yao hiyo ilianza kwa mabishano ya hoja katika mtandao wa Twitter kabla ya kukubaliana wakutane kushindanisha hoja hizo katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam ndipo Shangazi akamwambia ahakikishe na msosi wa kutosha unakuwepo.

Wawili hao wakiwa njiani kuelekea eneo la tukio.