Tuesday , 18th Oct , 2016

Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini (TFC) limepongeza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilolitoa wilayani Nachingwea hapo jana, la kufanyika haraka kwa maboresho ya menejimenti ya bodi ya Korosho,

Willigis Mbogoro

Uamuzi huo pia ulitaka uende sawia na kupitiwa upya kwa muundo na utendaji wa bodi zote za mazao nchini.

Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo Bw. Willigis Mbogoro amesema hayo katika mkutano wake na wanahabari jijini Dar es Salaam leo na kufafanua kuwa kwa kiasi kikubwa Waziri Mkuu Majaliwa ameamua kuondoa kero zote zilizokuwa zinavikabili vyama vya ushirika kupitia mwenendo mbaya wa bodi za mazao.

Mbogoro amesema alichokifanya Waziri Mkuu ni kumaliza kero zilizodumu kwa takribani miaka hamsini na ambazo zimekuwa chanzo cha vyama vingi vya ushirika kufanya vibaya kutokana na ubinafsi wa viongozi wachache waliopewa jukumu la kusimamia na kuendesha bodi za mazao.