
Mapambano ya ngumi yalifanyika kwa muda bungeni wakati wabunge wa chama cha mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters (EFF) walipotolewa kwa nguvu bungeni kwa kupiga makelele na kumzomea rais Zuma.
Hii ni mara ya kwanza kwa rais Zuma kufika bungeni tangu kutolewa kwa maamuzi mawili ya Mahakama yanayombana, yakiwemo ya kumtaka kurejesha fedha za umma alizotumia kukarabati nyumba yake binafsi.