Wednesday , 30th Apr , 2014

Umoja wa Wainjilisti Tanzania UWAKITA umeelezea kusikitishwa na kauli zilizotolewa kwenye bunge Maalum la Katiba ambazo hazina uhusiano na rasimu ya Katiba.

Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba. Umoja wa wainjilisti unamtuhumu Prof Lipumba kwa kuwaita wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuwa ni intarahamwe.

UWAKITA wameelezea hayo leo Jijini Dar-es-Salaam wakati wakitoa tamko lao kuhusu mjadala wa bunge maalum la Katiba kwa namna ulivyokuwa unaendelea.

Aidha, Wainjilist hao kupitia kwa Mwenyekiti wao, Bw. Samson Belegi wamemtaka Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF, kuwaomba radhi wajumbe wa bunge Maalum la Katiba na wananchi kwa ujumla kwa kauli yake aliyoitoa kwenye bunge hilo ya kuwaita Intarahamwe.