
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakipita kwenye daraja ambalo miundombinu yake iko hatarini kuharibiwa na mafuriko.
Baadhi ya wakazi hao ni wakazi wa Segerea Kisukuru huko Tabata ambao wapo hatarini kukosa mawasiliano ya barabara kufuatia baadhi ya maeneo ya barabara na daraja muhimu linalo unganisha eneo la Kimara kumeguka kwa kiasi kikubwa.
Wakazi hao wakizungumza na East Africa Radio wamesema kufuatia kuharibika kwa barabara katika maeneo hayo gharama za maisha zimepanda kutokana na kupanda kwa gharama za usafiri na kuongeza kuwa adhabu nyingine inayowanyemelea ni jinsi ya kupata maji safi kwa kuwa kwa muda mrefu sasa wanategemea Maboza ya maji ili kuwasambazia maji.
Naye katibu wa kamati ya wananchi ya matengenezo ya barabara Bw. Joseph Mwamnyange amesema pamoja na wananchi kuchangishana ili kukarabati baadhi ya maeneo korofi ili barabara zao ziendelee kutumika kuna baadhi ya maeneo yameharibika vibaya na hivyo kuhitaji nguvu za serika kuweza kuyakarabati