Monday , 22nd Feb , 2016

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki amemsimamisha kazi Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Bw. Said Nassor pamoja na wakuu wengine wawili wa matawi ya chuo hicho.

Mhe. Kairuki ameelezea uamuzi huo leo Jijini Dar es salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake, ambapo amesema watumishi hao wamesimamishwa kazi kutokana na utendaji usioridhisha pamoja na ubadhirifu wa fedha za umma.

Amewataja wengine waliosimamishwa kazi kuwa ni Bw. Sylvanus Ngata ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora na Bw. Mbwilo Joseph ambaye ni Kaimu Mkuu wa chuo kwa upande wa Utawala na Fedha..