
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Kupitia ofisi ya Mkuu wa mkoa, Mrisho Gambo, imejipanga kukabiliana na changamoto hiyo isijirudie tena kwa kuanza ujenzi wa shule mpya za sekondari katika maeneo yaliyoonekana yana uhitaji.
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa shule moja mpya ya sekondari inayojengwa kwenye Kata ya Olasiti jijini humo mkuu wa mkoa Mrisho Gambo amesema changamoto hiyo imesababisha mkoa kuchukua hatua za uwashirikisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha wanapata shule mpya za mfano na zenye uwezo.
Hatua hii inawashirikisha wananchi wa kawaida ambao wanaonekana kuunga mkono ujenzi huo kwa kila mtu na anachokiweza ili shule ikamilike.
Katika kipindi cha mwaka 2018 takribani wanafunzi elfu kumi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika mkoa wa Arusha walikosa nafasi hali iliyolazimu wanafunzi kupangwa kwa idadi kubwa katika madarasa tofauti na maelekezo ya wizara ya elimu.