
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga, Taasisi ya Saratani Ocean Road Jijini Dar es salaam Dr.Crispin Kahesa
Akizungumza katika kipindi cha EAST AFRICA BREAKFAST BREAKFAST Dkt. Kahesa amesema mfumo wa maisha kwa sasa kutokana na vyakula vya mafuta ambavyo watu wengi wanavipendelea kutokufanya mazoezi, na matumizi ya vilevi kupindukia na uvutaji wa sigara umekuwa ni chanzo kikubwa cha ongezeko la wagomjwa wa saratani.
“ Mfumo wa maisha ni chanzo pia kwa sasa kinachoongeza idadi yan wagonjwa wa saratani, ni vyema watu wakajenga utamaduni wa kukagua afya mara kwa mara pamoja na kufanya mazoezi, kula matunda pamoja na kunywa maji ya kutosha ili kujikinga na maradhi ya saratani” Amesema Dkt. Kahesa.
Aidha Kahesa ameongeza kuwa ugonjwa wa saratani ukigundulika mapema, mgonjwa anaweza kupaata matibabu na kuwa salama kabisa au kupata matibabu ambayo yanaweza kumfanya akawa salama zaidi kuliko kukaa hadi ugonjwa unajijenga na hali ikiwa mbaya ndipo mtu anajitokeza.
Pamoja na hayo Dkt. Kihesa amewataka wananchi kuepuka kuamini imani za kishirikina kwenye ugonjwa wa saratani bali kila wanapoona wana dalili zisizo za kawaida katika miili yao na kwenda kwenye vituo vya afya kkufanya uchunguzi wa awali mapema
