Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako
Akizungumza kwa Naiba ya Rais Magufuli katika uzinduzi wa meli ya Logos Hope inayouza vitabu kutoka Mexico Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema usomaji wa vitabu husaidia maarifa katika kupambana na Umasikini.
Prof. Ndalichako amewataka watanzania hasa waishio Jijini Dar es Salaam kutumia Fursa ya uwepo wa meli hiyo ya vitabu kujisomea ili kupata maarifa zaidi huku akisisitiza utamaduni wa kujisomea iwe ni kawaida ya Watanzania.
Meli hiyo ya Logos hope ambayo imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaama ikiwa na lengo kubwa la kuwahamisha Watanzania katika usomaji wa vitabu ambapo kuna aina ya vitabu zaidi ya vitabu elfu tano katika meli hiyo.
Vitabu vinavyopatikana katika meli hiyo kutoka Mexico ni pamoja na vitabu vya elimu vya shule, Upishi, michezo, Kamusi na Atlasi.
