Thursday , 12th May , 2016

Takwimu zinaonyesha kuwa nchini Tanzania kwa wastani muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa 40 wakati ilitakiwa muuguzi mmoja ahudumie wagonjwa 6 hadi 8.

Wakizungumza na East Africa Radio kwa nyakati tofauti wauguzi wamesema iwapo wakiwezeshwa na wakijengewa mazingira mazuri yakutosha kufanya kazi zao vizuri basi wanaamini wataweza kuleta mabadiliko makubwa sana katika utoaji huduma bora katika sekta ya afya nchini.

Wamesema katika tafiti zilizofanyika ambazo zimeangalia kipi bora kati yakuboresha mazingira ya kazi kwa muuguzi au kuongeza idadi ya wauguzi, tafiti hizo zimebaini vyote vinaumuhimu katika kutoa hudumaza afya na pindi vinapopungua au kukosekana kabisa husababisha athari katika sekta ya afya kwakuwa kama mazingira ya kazi sio mazuri basi hata wauguzi hawawezi kufanya kazi zao vizuri.

Wamesema kuna baadhi ya vitengo vya magonjwa ambavyo vinahitaji mgonjwa ahudumiwe na wauguzi wawili kama vile vya akili na vile vya wagonjwa mahututi lakini havifanyi hivyo nakupelekea wauguzi kufanya kazi katika mazingira magumu na kuongeza gharama.

Wakati huo huo Wakunga wamekemea wanasiasa wanaowapandikiza chuki wananachi kuhusu wauguzi kwani sio wauguzi wote ambao wanakua sio waaminifu kwa wagonjwa na kwa jamii kwa ujumla na wame kemea wauguzi wenzao wanaofanya kazi kinyume na makubalianao ma sheria za kazi za uuguzi.

Wamesema ni vizuri sasa kwa serikali na waajiri wote kuhakikisha kuwa mazingira ya kazi ya muuguzi ni mazuri na yanamuunga mkono katika utendaji wa kazi zao kwa ujumla.

Kila tarehe 12 ya mwezi wa 5 ni siku ya Wauguzi Duniani na kwa mwaka huu siku hii imebewa kauli mbiu isemayo "Wauguzi nguvu ya mabadiliko, uboreshaji wa uthibiti wa mfumo wa afya".