Wednesday , 12th Oct , 2016

Wakala wa vipimo nchini (WMA) imewataka wafanyabiashara wote wanaojihusisha na biashara ya jumla na rejareja ya gesi, kuhakikisha wanatumia mizani iliyopitishwa na kuthibitishwa na wakala kupimia uzito wa mitungi ya gesi wanayoiuza kwa wateja wao

Mitungi ya gesi

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt. Ludovick Manege ametoa agizo hayo jijini Dar es Salaam kufuatia kile alichoeleza kuwa ni kuibuka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiwaibia wateja kwa kuwauzia mitungi ya gesi iliyo chini ya ujazo.

Kuhusu adhabu inayowakabili wafanyabiashara wanaokiuka maagizo hayo, Dkt. Manege amesema kumekuwa na mapungufu ya kisheria yanayochochea kuendelea kwa vitendo vya uchakachuaji wa gesi kwani adhabu ya wanaokiuka sheria hiyo ni faini ya shilingi elfu kumi, kiasi alichoeleza kuwa ni kidogo ikilinganishwa na ukubwa wa kosa.