Saturday , 27th Aug , 2016

Serikali imesema itawanyanganya ardhi wawekezaji waliohodhi ardhi ya Tanzania bila kuiendeleza.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ambapo amewataka kuyaendeleza maeneo hayo haraka kabla serikali haijaamua vinginevyo.

Waziri Lukuvi pia amewaagiza wawekezaji wanaohitaji ardhi kwa ajili ya shughuli za uwekezaji ikiwemo viwanda, kuacha kununua ardhi moja kwa moja katika vijiji, na badala yake kutuma maombi katika wizara yake au kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Amesema ili kumaliza migogoro mbalimbali ya ardhi ambayo hutokea mara kwa mara kati ya wananchi na wawekezaji, hivi sasa serikali inaandaa muongozo maalum ambao utaeleza namna sahihi ya utumiaji na ugawaji wa ardhi.

Amekitaka Kituo cha Uwekezaji (TIC) kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhudumia wawekezaji hususani katika masuala ya ardhi kwa kushirikiana na wizara hiyo