
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Katikati) amesimikwa Kiongozi wa Machief katika Wilaya ya Mbozi Chief Muleshwelwa Nzunda.
Mh. Hasunga ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi ambao walijitokeza wakati akisimikwa kuwa 'Chief Nzunda' kutokana na majukumu makubwa anayoyafanya katika wizara yake sambamba na uwajibikaji katika Jimbo lake la Vwawa.
Amesema kwamba serikali ipo tayari kuyafanyia kazi malalamiko ya wakulima kuhusu bei za pembejeo za kilimo ili kuwa na unafuu wa gharama zitakazoendana na uwezo wa wananchi.
Mhe. Hasunga ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwani ndiyo silaha pekee ya maendeleo.
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Mhe. Dkt John Pombe Magufuli anatuhimiza kufanya kazi kwa bidii ili kupambana vizuri katika hali zetu kiuchumi ni wazi kuwa lazima tukubali kuweka siasa kando," - Hasunga.
Aidha Mh. Hasunga amewataka wananchi kuiunga mkono CCM kwa kuwa ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa.