
Adili Chapakazi
eNewz ya EATV ilizungumza naye na kusema kuwa wasanii wengi hivi sasa wanapiga mizinga jambo linalomfanya kuweka wazi kuwa hatafanya kazi isiyo na faida, au isiyo na malipo
"Siwezi kufanya kazi ambayo inakuwa haina hela inaishia tu ni ujiko wasanii wengi wamekuwa wanapiga mizinga, msanii anaweza akaja kwako akakuomba mfanye video ya shilingi laki mbili halafu akaondoka na kusema kuwa kafanya au kalipa milioni mbili kwa hiyo wasanii wengi wabadilike"
Akizungumzia ujio wake mpya amesema kuwa hivi saa amerudi kiutofauti kwa kuwa ameona kuna fursa ya kupata faida.
"Nimerudi na nina angle yangu ninayojua, narudi nayo na sifanyi kazi kwa ujiko na nimerudi kwa sababu naona kuna opportunity mbalimbali ikiwemo kutengeneza vipindi". Alisema Adili.
Mtazame hapa kwenye show ya eNewz