
Pichani, Afande Sele
Afande amesema hayo yakiwa yamebaki masaa machache kumalizika kwa mwaka 2018 ambapo ameainisha kwamba yeye ataupokea mwaka akiwa kanisa la Romani Katoliki kwa kuwa ndilo dhehebu linaloishi kwa sasa moyoni mwake.
"Mwaka mpya, imani na jina jipya kutoka Selemani hadi Selestine itapendeza sanaaaa....na kama haitoshi nimemuambia shemeji yangu Mama Maria 'The ticha' kuwa ndani ya mwaka huu unaokuja yaani 2019 najisikia kuoa tena, na itanifaa zaidi kupata mke mkatoliki safi ili tujenge familia bora itakayofunikwa na ulinzi wa damu ya Yesu"
Afande Sele, 'Seleman Msindi' ambaye ni baba wa watoto wawili, mwaka 2016 aliwahi kukiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa hana mpango wa kuoa mapema kwa kuwa ana jukumu kubwa la kuwalea watoto wake ambao mama yao alifariki dunia 2014.