Wednesday , 26th Mar , 2014

Mwigizaji mzaliwa wa Somalia anayeshikilia rekodi ya kuwania tuzo za Oscar Barkhad Abdi,
ameripotiwa kuwa katika hatari ya kufukuzwa huko nchini Marekani kutokana na rekodi mbalimbali za uhalifu.

Barkhad Abdi

Abdi katika historia yake anmewahi kupatikana na dawa za kulevya, kudanganya jina na kufungwa jela mara mbili mwaka 2012.

Abdi ambaye amejipatia umaarufu kupitia ushiriki wake katika filamu ya Captain Phillips ambayo imemuwezesha kuwania na kushinda tuzo mbalimbali za kimataifa, alijikuta akiingia matatani na maafisa uhamiaji akiwa anarejea Marekani kutoka Ulaya ambapo alikwenda kupokea tuzo ya BAFTA.

Imefahamika kuwa, kwa sasa Abdi anajishughulisha na kutengeneza filamu mpya ambayo anaiongoza mwenyewe, na bado taarifa za uwezekano wa yeye kutimuliwa nchini humo na maafisa uhamiaji hazijaweza kuthibitishwa.