Thursday , 6th Apr , 2017

Msanii maarufu wa bongo movie ambaye mara nyingi hucheza uhusika wa kupigana amewashauri wasanii wa bongo movie kuwa na njia mbadala ya kuingiza kipato na badala ya kutegemea sanaa pekee.

Mobby

Akiongea kupitia eNewz Mobby amesema wasanii wengi wakishapata umaarufu wanaacha kazi zao walizokuwa wakizifanya awali, wanaacha kutembea kwa miguu kwa kusema kwamba wameshakuwa ma-star hali inayowapelekea kushindwa kufanya kazi zao binafsi. 

Pia Mobby aliwashauri waigizaji wenzake kurudia kazi zao za asili ili kuweza kuepusha kashfa za hapa na pale kwani mpaka wasanii wa kiume wengi wao wanakuwa 'marioo' yaani wanakuwa ombaomba jambo ambalo amesema ni aibu na linafanya watu maarufu kudharauliwa.

Akimalizia, Mobby alisema "Kweli mimi ni star lakini siwezi kuacha kazi ambayo imenilea kwa kuwa sanaa imekuja baada ya kuwa na kazi yangu ambayo ilikuwa inanilea na ukiniona kwenye gazeti ujue nafanya promo ya kazi ya yangu na siyo vinginevyo, nawasihi wanaopenda kashfa waache kujipotezea muda maishani mwao".