Thursday , 29th Jan , 2015

Mtayarishaji video mahiri kutoka Kenya, Kevin Bosco Junior amesema kuwa, kutokana na kukua kwa kasi kubwa kwa soko la utayarishaji video Afrika Mashariki kwa upande wake anaona ni vyema kuunganisha ujuzi kwa nchi hizi ili kuweza kujifunza zaidi.

Mtayarishaji wa video za wasanii nchini Kenya Kevin Bosco Jr

Kevin amesema kuwa juu ya suala la umoja, vilevile tofauti na watayarishaji video wengine anafurahi kuona wasanii wakifunguka na kutoka nje ya mipaka ya nchi zao kwenda kufanya kazi bora nje ya mipaka, akisisitiza umoja kwa Afrika Mashariki ambao utawavuta wasanii hawa kutafuta ubora huo hapa hapa.