Rapa Fareed Kubanda
Fid Q aliamua kumchana shabiki huyo na kumweleza kuwa siku nyingine asimwite tena jina hilo la 'Mungu' kwa kuwa siku zote katika maisha Mungu ni mmoja tu na hakuna mwingine zaidi ya yeye aliyeumba dunia na vitu vyake vyote.
"Bonniephace Mungu ni mmoja tu .. So please usiniite hilo jina tena. Mungu ndiye kaniwezesha niwe na maukali hayo mimi siyo lolote bila yeye pia kakuwezesha wewe upeo wa kuweza kuyashtukia. Naomba tujitahidi kulitukiza jina lake milele. Amina" alindika Fid Q
Mbali na hilo mashabiki wengi walionesha kumuunga mkono shabiki huyo aliyemwita Fid G Mungu wa Hip Hop na kusema msanii huyo kwa Bongo hakuna wa kufanana naye kwani uwezo wake ni mkubwa sana japo wanakiri kuwa hakupaswa kutumia jina hilo la Mungu.
Tazama hapa mazungumzo yalivyokuwa: