.jpg?itok=109QJ8fG×tamp=1492591627)
Azma Mponda
Azma Mponda alisema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo na kusema baada ya kuona muziki haumpi maslahi yoyote zaidi ya kumrudisha nyuma aliamua kuchukua vyeti vyake na kutafuta kazi ili afanye kazi kulingana na fani yake.
"Nilikaa kwenye industry ya muziki Tanzania kwa muda mrefu ilifikia wakati nilitaka kukata tamaa sababu niliona napoteza muda mrefu harafu nimesoma zangu, vyeti vipo mtu vimekaa tu ndani, nikawa naona washikaji zangu ambao walikuwa wakiniheshimu nakuta wapo ofisini nikasema ngoja tu nitafute kazi, kwa hiyo nikasema kwanini tu nisiende Kenya nilipofika Kenya nikakuta muziki wangu kule umefika mbali sana na nikapokelewa vizuri sana" alisema Azma Mponda
Azma Mponda anasema hapo ndipo ulipokuwa mwanzo mzuri wa muziki wake na mafanikio ya muziki wake kwani tayari Kenya alikuwa na nafasi nzuri zaidi.
"Mtu wa kwanza kufanya naye kazi Kenya alikuwa Khaligraph Jones watu wakanipokea katika ukubwa ambao sikuwahi kuwa nao, nikaona hapana ngoja nifanye huu muziki, ndiyo hapo mabadiliko yalipoanza kutokea na mimi mwenyewe nikapata ile hamasa ya kuendelea kufanya muziki, kikubwa matumizi ya lugha ya Kiswahil kule ndiyo yalinipa nafasi nzuri" Azma Mponda