Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Irene Uwoya ataja kilichomkosesha ubunge CCM

Sunday , 26th Feb , 2017

Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefafanua sababu za kutopitishwa na chama chake cha CCM kuwa mbunge wa Viti Maalum vya wanawake, na kusema kuwa kilichomuangusha ilikuwa ni kura za Rais kuwa chache.

Irene Uwoya

Uwoya alikuwa akijibu maswali ya wapenzi na mashabiki zake LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, ambapo swali la kwanza kabisa kuulizwa, lilihoji sababu za yeye kutemwa kwenye ubunge ndani ya CCM na kama bado ana ndoto za kuwa mbunge.

Katika majibu yake, Uwoya alisema bado ana ndoto za kuwa mbunge huku akiweka wazi kuwa yeye hakutemwa na wala hakushindwa katika kinyang'anyiro hicho isipokuwa nafasi yake kuwa mbunge ilikuwa inategemea idadi ya kura ambazo angepata aliyekuwa mgombea urais

"Niligombea kupitia upande wa vijana na nilishinda, sikushindwa wala sikutemwa, kwanza kwa mkoa wa wangu wa Tabora nilipata kura za kutosha tena nilikuwa namba moja kabisa, kwenye taifa pia nilifanikiwa kuwa kwenye majina 10 ambayo yalikuwa yanategea kura Rais, kama Rais angepata kura nyingi basi tungechukuliwa wote, lakini kwa kura alizopata Rais ilibidi wachukuliwe 6, kwahiyo mimi sikushindwa, mimi nilishinda lakini asilimia za kura za Rais ndiyo hazikutosha". Alisema Uwoya

Kuhusu nafasi ambayo angependa kuteuliwa kwa sasa katika serikali ya awamu ya tano, Uwoya amesema Mungu ndiye anayejua, na wakati ukifika anaweza kupata nafasi yoyote kwahiyo hawezi kujipangia. 

Huyu hapa Uwoya akifafanua.....

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine