Thursday , 26th Apr , 2018

Ikiwa zimepita siku chache tokea alipofariki na kuzikwa msanii wa BongoFleva Jebby ambaye alijipatia umaarufu mkubwa enzi za uhai wake na wimbo kama 'Swahiba' kimeibua maswali mengi kwa watu wake wa karibu huku wengine wakidai kifo chake kimetokana na imani za ushirikina.

Akizungumza na eNewz kutoka EATV rafiki wa karibu na marehemu Jebby ambaye pia ndiye aliyekuwa akimuuguza kwa kipindi kirefu wakati alipokuwa Jijini Dar es Salaam Francis Vitus na kusema Jebby kabla ya kufariki alikuwa anauguwa mara kwa mara na muda mwingine mpaka anazidiwa lakini dawa alizokuwa amepewa hospitali zilikuwa zikimsaidia kwa kiasi fulani na kurudi katika hali yake.

"Kuna kitu kilikuwa kinanistua cha yeye kutokwa na damu nyingi maeneo ya puani, nilikuwa namuuliza inasababishwa na nini alikuwa anajibu hajui ila anaona zinatoka tu ila kitendo cha damu kukatika anakiona cha kawaida na kufurahi", amesema Vitus.

Pamoja na hayo, Vitus ameendelea kwa kusema "suala la kifo chake kuhusishwa na imani za kishirikina sina imani nalo zaidi ingawa mimi mwenyewe nilikuwa namuuliza lakini alikuwa ananikwepa na kuniambia kama kweli ni vitu vya kishirikina yeye anamuachia Mungu maana kama kufa bora kufa lakini yeye anajiona sawa tu. Ila nilishindwa kuelewa kwa mtu kama yeye nyumbani kwao kwenye msiba kusiwepo na hata turubai nikauliza lakini sikupata jibu".

Mtazame hapa chini rafiki wa marehemu Jebby, Francis Vitus akielezea zaidi....