Thursday , 21st May , 2015

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba ametangaza kukamilika kwa taratibu zote za maandalizi ya tuzo kubwa za filamu TAFA 2015, tukio litakalofanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyrere, kuanzia saa 2 usiku.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba

Katika Mkutano wake na waandishi wa habari Mwakifwambwa ameeleza kuwa, wageni kutoka nje ya nchi wamekwishaanza kuwasili kuanzia leo kwa ajili ya tukio hilo kubwa, ambalo pia litahusisha burudani ya muziki na vichekesho kutoka kwa wasanii King Kikii, Barnaba, Mwasiti, Oscar Nyerere na wengineo.

Tiketi za tukio hilo zinapatikana kwa shilingi 50,000 kwa viti vya kawaida na laki moja kwa VIP katika maeneo mbalimbali ikiwepo ofisi za EATV Mikocheni, kama anavyoeleza zaidi Mwakifwambwa.