Saturday , 6th Sep , 2014

Maandalizi ya Onesho kubwa kabisa la Kilimanjaro Music Tour, kwa mujibu wa waratibu wanaosimamia shughuli hii eneo la tukio, yamezingatia usalama na muziki wa kiwango cha kimataifa.

Proffesa Jay kwa Stage

eNewz imebaini haya moja kwa moja kutoka, Leaders Club Kinondoni baada ya kuzungumza na Daniel Ngowi, Afisa anayesimamia mradi huu ambapo amesema kuwa, kutakuwa na polisi zaidi ya 100, vikosi vya Ninja na Security wa kawaida pia taa za kutosha kupambana na giza ambalo wahalifu hupenda kutumia kufanya mambo yao.

Sound Engineer Bwana Abraham Ngumuo amesema kwa yeyote atakayehudhuria onesho hili atakuwa salama kabisa na pia atajifunza mambo mapya juu ya kiwango cha kimataifa cha maonesho katika upande wa ulinzi na usalama.