Sunday , 7th Sep , 2014

Tamsaha Kubwa la Muziki, Kilimanjaro Music Tour limamalizika kwa mafanikio makubwa katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi kutoka ndani na nnje ya jiji la Dar es Salaam.

Professa Jay na Mdogo wake wakilishambulia jukwaa

Tamasha hili limeshuhudia wasanii wakali kabisa wa muziki hapa Tanzania wakipanda jukwaani na kutoa burudani ya aina yake , shughuli nzima ikifunguliwa na Mashujaa Band, wakifuatiwa na Jose Mara na Bendi yake Christian Bella na vile vile Bibie Khadija Kopa.

Mashambulizi juu ya Jukwaa yakaendelezwa na wasanii Rich Mavocal na madansa wake, Vanessa Mdee na madansa wake, Ommy Dimpoz na madansa wake, pia Ben Pol ambaye mbali na kufanya onyesho kali kabisa alimtambulisha kwa mashabiki msanii mpya kabisa wa R&B anayekwenda kwa jina Herry Muziki.

Tamasha hili liliongezeka hamasa na burudani pale Proffesa Jay alipopanda jukwaani kutumbuiza akifuatiwa na AY ambaye alilishambulia jukwaa na MwanaFA na baadaye show kufungwa na onyesho la nguvu kabisa kutoka kundi la Weusi.

Onyesho hili lilishuhudia upendo wa kutosha hata baada ya kunyesha kwa mvua mara kadhaa, hali ambayo haikuweza kukatisha mzuka wa mashabiki kuendelea kuburudika na hata kufikia wakati wa kumaliza show takriban majira ya saa 10 alifajiri, mashabiki hawa waliofika kwa wingi walikuwa na hamu ya kuendelea kuburudika.

Kwa kulitazama onyesho hili kwa uhakika, endelea kutazama EATV tinga lako namba moja kwa vijana.