Friday , 13th May , 2016

Komedian kutoka Bongo Mohammed Abdallah almaarufu Kinyambe amezikwa mkoani Mbeya baada ya kufariki usiku wa Jumaatano ya tarehe 10

Komedian kutoka Bongo Mohammed Abdallah

Kinyambe alikuwa ni komedian mwenye style tofauti ya Uigizaji na taarifa zilizopo ni kwamba amefariki kwa ugonjwa wa kujaa maji kwenye mapafu japokuwa inaaminika alikuwa hatumii pombe wala sigara.

Msiba wake ulihudhuriwa na wasanii wengi hasa wa komedi na kuiambia Enewz kuwa Kifo chake kimeacha pengo kubwa katika upande wa komedi, kwakuwa hakuna atakaeweza kucheza kwa style yake.