
Lupita Nyon'go (katikati)
Kituo pia kina na jumba la sinema la nje, pamoja na jukwaa la shughuli mbalimbali za maonesho ya sana.
Lupita mwenye asili ya Kenya ametua nchini Uganda hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya upigaji picha filamu mpya iliyobatizwa jina ‘Queen of Katwe’ ambayo inafanyiwa kazi kwa umakini na muongozaji mahiri Mira Nair kutoka kampuni ya Maisha Film Lab.
Lupita amekuwa akijipanga vyema kwa kuanza kuigiza katika filamu hiyo mpya ambayo inahusu msichana aliyetokea katika maisha duni mjini Kampala ambaye baadaye alikuja kuwa nyota katika mchezo wa drafti ambapo Lupita ataigiza uhusika wa mama wa msichana huyo aitwaye Phiona.