Tuesday , 23rd Aug , 2016

Kundi la Tatanisha Crew kutoka eneo la Mabibo Jijini Dar es Salaam limesema linaridhishwa na namna ambavyo majaji wa shindano la Dance100% wanatoa alama vizuri bila kuwa na upendeleo wowote kulingana na uwezo wa kundi jambo ambalo linawatia moyo kati

Kundi la Tatanisha Crew linaloshiriki Dance100%

Akizungumza na EATV Mwenyekiti wa kundi hilo Thomas Paul amesema kitendo cha majaji kuwa na maamuzi sahihi na kueleza kila kundi wapi limefanya vizuri na vibaya kumewafanya kuwa na imani kubwa na majaji na kuongeza hamasa ya mazoezi ili kundi lao liweze kuibuka na ushindi.

“Sisi tunafanya mazoezi kwa hali ya juu kujiandaa na hatua ya nusu fainali kwa kuwa tuna imani kubwa na majaji kwamba wanatenda haki kulingana na kundi linavyoonesha uwezo na sisi tutakuwa tayari kwa matokeo yoyote kwa kuwa tunawaamini kwa namna wanavyo chambua kundi moja moja kulingana na vigezo vya shindano” Amesema Thomas Paul

Kwa upande wake mmoja wa majaji wa shindano hilo Jaji Super Nyamwela amesema katika shindano la Dance100% hakuna upendeleo wowote na makundi yote yapo sawa na yameshaelezwa vigezo ambavyo vinatakiwa ili kundi liweze kufuzu shindano hilo.

“Hakuna kundi ambalo linaweza kusema kuna upendeleo kwa kuwa mambo yote tumeshawaeleza na kuwafundisha kwa mfano kuvaa sare, kutotafuna kitu wakati wa kucheza, kuwa na usawa, kucheza kwa kuendana, kutunza muda, pamoja na kuwa wabunifu katika nyimbo wanazocheza”- Amesema Nyamwela.

Majaji Dance100%
Tags: