
Mansu-Li
Mansu-Li ameiambia eNewz kuwa traki hiyo mpya ambayo ndio kwanza imeachiwa rasmi kupitia stesheni mbalimbali nchini imefanyiwa kazi katika studio ya Tongwe Rec chini ya maprodyuza Geof Master na Yuddy.
Aidha, rapa huyo amesema kuwa hii ni ngoma iliyopo ndani ya project yake Adam Juma, iliyobatizwa jina 'ONE LIFE' iliyomuwezesha Mansu-Li kukutana naye Damian na kushirikiana kwa pamoja kutoa ngoma hii.
Pata kionjo kifupi cha trak hii mpya kutoka kwake Mansu-Li featuring Damian Soul, 'Kila Sababu'.