Wednesday , 26th Mar , 2014

Mwanzilishi mwenza wa tovuti ya Jamii Forums, Maxence Melo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media leo hii ameweza kuingia Kikaangoni Live ya Facebook EATV.

Maxence Melo katika 'Kikaango' leo

Zoezi hili limetoa fursa kwa umati mkubwa watumiaji wazuri wa tovuti ya Jamii Forums kufahamu mambo mhuhimu ikiwepo sababu ya kuanzishwa kwa Jamii forums? Faida na hasara zake ni zipi, na pia Maisha yake ikiwepo burudani anazopenda.

eNewz tulipata fursa ya kuhojiana na Maxence Melo baada ya zoezi hilo na kuzungumza nae ambapo amesema amefurahi kushiriki Kikaangoni na amegusia swala la wasanii na mitandao ya Jamii na kusema kuwa wana nafasi kubwa kwao kutumia mitandao hii 'kuji-brand' ambapo yeye na timu yake wanawakaribisha wote kwaajili ya kuwasaidia kutumia mitandao hii ipasavyo bila gharama yoyote.

Baada ya kumaliza na Maxence Melo sasa kaa tayari kuchat na staa mwingine mkali juma lijalo tena katika Kikaangoni Live, ambayo inakujia kupitia www.facebook.com/eatv.tv pekee.