Tuesday , 26th Jan , 2016

Msanii Linex amesema mwaka huu utakuwa mwaka wake wa kufanya biashara ya muziki kuliko miaka yote aliyowahi kufanya muziki.

Linex ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kueleza kuwa uongozi alionao sasa hivi wana pesa za kutosha kuweza kuwekeza zaidi kwenye muziki.

“Biashara yangu ya muziki mwaka huu itachange kwa sababu nina management ambayo ipo strong, yani ni watu ambao ukimpa plan ya business anaweka chapaa, means kwamba nitafanya biashara ya muziki mwaka huu kuliko mwaka wowote ambao nimefanya biashara ya muziki”, alisema Linex.

Pia Linex ambaye kwa sasa anaendelea kufanya poa kwenye game kwa wimbo wake mpya unaoitwa “kwa hela”, amesema yeye bado ni kiboko kwenye game, kwa kuwa anafanya muziki kwa namna ya peke yake.

“Mi sikurupukagi vitu vyangu navipeleka kwa mipango, unajua mi nikitoaga nyimbo lazima inatoka inasound tofauti na nyimbo ambazo zinarotate kwenye radio, huwa sitoi ngoma halafu ikawa inafanana beat na nyimbo ya mtu fulani, au na melody na mtu fulani au maneno, sana sana mi ndo naanzisha maneno, huwezi kusikia line zangu zinafanana na line za mtu mwengine hata siku moja”, alisema Linex.