Thursday , 16th Oct , 2014

Msanii wa muziki Meninah la Diva ametoa ya moyoni kuwa, kutokana na vijana wengi wa umri kama wak

Meninah

Msanii wa muziki Meninah la Diva ametoa ya moyoni kuwa, kutokana na vijana wengi wa umri kama wake kwa sasa kujihusisha kwa wingi katika mahusiano yasiyo na uaminifu, wamekuwa katika nafasi kubwa ya kudumbukia katika maradhi mbalimbali na kukosa malengo.

Meninah amesisitiza kuwa, kutokuwa na malengo kumekuwa ndio tatizo kubwa linalowapoteza wengi, huku akisema kwa upande wake amefanikiwa kuvuka majaribu mbali mbali kutokana na muongozo wa malengo yake.