Monday , 10th Apr , 2017

Msanii anaye tamba na wimbo wa 'Garagasha' Azma Mponda amedai yeye ndiye chimbuko la msanii Young killer ambapo baada ya kumshirikisha katika wimbo wa 'Saa mbovu' ndipo msanii huyo nyota yake ilianza kung'ara na kupata fursa ya kuonekana

Azma (Kushoto) na Young Killer (Kulia)

Akizungumzia katika maisha yake ya kuweza kutafuta njia ya kujulikana katika bongo fleva Azma amesema katika utafutaji alijikuta anafanya wimbo ulioitwa "Saa Mbovu japo haukufaya vizuri lakini ndiyo ulikuwa chanzo cha rapa anayesumbua kwa sasa kuonekana na wadau mbalimbali wa muziki.

Hata Azma amefunguka kuwa baada ya ngoma kutofanya vizuri Belle 9 alimuomba wafanye kolabo huku akidai ngoma ya saa mbovu angekuwa yeye ni DJ au mtangazaji angekuwa anaipiga mara kwa mara sababu ilikuwa na sifa zote za kuwa 'hit song'.

"Mimi ni chimbuko la Young Killer na mimi ndiye niliyemtoa wadau wakamuona. nilifanya naye wimbo wa saa mbovu haukufanya vizuri lakini yeye akatoka ni kitu ambacho kinaishi kwenye historia ya maisha yangu ya muziki. Huwezi kuamini japo wimbo haukufanya poa Belle 9 alinitaka tufanye wimbo sema nilichomoa kwa sababu nikuwa bado sijajua niimbe kuhusu nini na bado sikuwa hata na hit song kwenye redio tofauti na yeye alikuwa tayari ni mkubwa"- Azma

Azma Mponda

Aidha msanii huyo amedai kuwa wimbo wa Astara vaste aliofanya na Belle 9 ni wimbo ambao alirudi kuomba kolabo baada ya kuhit nchini Kenya na akiwa tayari amekwishafanya kazi na Khaligraph Jones na baada ya kufanya vizuri akaona fusra ya kuachia 'Garagasha'.