
Nancy ambaye ni mke wa msanii Roma.
Akipiga stori na Jr kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Nancy amefunguka mengi ikiwemo jinsi alivyokabiliana nalo tukio hilo, na jinsi alivyokuwa akiumia baada ya mumewe kugundulika kuwa ametekwa.
Nancy amesema kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza zaidi ni pale mtoto wake alipokuwa akimuulizia baba yake na hajui aliko na kama yupo salama au la, na pia kitendo cha watu kusema tukio la Roma kutekwa lilikuwa ni maigizo, wakati amerudi akiwa na majeraha.
Msikilize hapa chini akiongea na Jr Junior kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio.