Sunday , 5th Feb , 2017

Msanii wa bongo Fleva Kutoka Makomando Muki ameamua kumuanika wazi mchumba wake ambaye kwa sasa ni mjamzito.

Muki

Msanii huyo kutoka kundi la Makomando amezungumza na eNewz ya EATV na kuweka wazi kuhusu ujauzito huo na kukiri kuwa huyo atakuwa ni mtoto wa pili kutoka kwake.

Je, mwanamke huyu ndiye aliyempatia mtoto wa kwanza au?, Jibu alilotoa ni kwamba siyo mwanammke huyo bali ni mwingine na kwa sasa anategemea kupata mtoto wa pili hivi karibuni.

“Nina mtoto mmoja na mwingine anakuja lakini mama ni tofauti na wamepishana miaka lakini bado hajafikia umri wa kwenda shule na siishi naye nyumbani bado kwa sababu bado nina mambo yangu mengine, ila huyu mwenye ujauzito ninaishi naye kwa sababu mwananmke anavyokuwa mjamzito akili inakuwa siyo yake na ananihitaji niwe karibu naye ninavyokaa naye ndiyo tunaongeaga vitu vingi na hii haijawa official kwa sababu hata wazazi bado hatujaoana bado” Amesema Muki

Muki na Fred ni moja kati ya wasanii ambao wameunda kundi la Makomando