
Shamsa Ford
Shamsa Ford anasema mara nyingi wanawake wanapenda kuwa na mwanaume ambaye ana heshima na mapenzi ya dhati lakini pia mtu ambaye anajitoa kwa mpenzi wake kwa lolote pasipokuwa na wasiwasi wowote.
"Wanawake siku zote huwa tunapenda heshima, kupendwa, kuthaminiwa na kupewa kipaumbele na wanaume zetu. Mwanamke mwenzangu ukiona mwanaume haeleweki, hakuthamini, mapenzi mpaka muwe wawili ndiyo anakuonesha ila mbele za watu anazuga kama yupo na bibi yake basi ujue huyo si wako. Mwanaume anayekupenda na kukuthamini atatamani dunia nzima ijue kama anakupenda. Atakupenda na kukuthamini muda wowote bila kikwazo" Aliandika Shamsa Ford
Shamsa Ford ni mke wa mfanyabiashara Chid Mapenzi ambaye naye ametajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika sakata la dawa za kulevya.
Shamsa na mumewe Chid Mapenzi