Monday , 31st Dec , 2018

Mwaka 2018 huenda ukawa ni mwaka mzuri zaidi kwa baadhi ya wasanii wa Bongofleva ambao wamepata muda wa kusikika zaidi kupitia ngoma zao na hatimaye kupata kipato ambacho kimewasaidia kufanya mambo makubwa.

Kushoto ni msanii Nandy na kulia ni Dogo Janja.

Katika wasanii hao huwezi kuacha kumtaja mwanadada Nandy ambaye kupitia 'hit song' zake kama, Ninogeshe, Subalkheri na Aibu, ameweza kutengeneza mkwanja mrefu ambao ameutumia kujenga nyumba na kuwakabidhi wazazi wake.

Kupitia 'Instagram' Nandy ameweka picha ya nyumba hiyo na kuandika haya, ''Mungu wangu na Baba yangu najua nakukosea sana kama binadamu na kama kijana ila nikipiga goti unajua namaanisha kutoka moyoni mwangu na unajua hakuna ninaye mtegemea zaidi yako''.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

A small gift for my parent this year 2018... Zawadi ndogo ya wazazi wangu mwaka huu 2018.. . . WISDOM IS POWER

A post shared by NANDY (@officialnandy) on

''Asante kwakunipa uvumilivu, unyenyekevu, katika maisha yangu hasa kipindi hiki cha mwaka 2018!! Asante kwa hii zawadi ndogo ya wazazi wangu najua hii ni ndoto ya kila kijana mwenye kutafuta!!! Ni kila ndoto ya mwanadamu yoyote duniani kuona wazazi wake wako na furaha na ndiyo baraka zenyewe'', - Nandy.

Mwanzoni mwa mwezi Desemba msanii mwingine wa Bongofleva Dogo Janja a.k.a 'Janjaro', ambaye mwaka 2018 pia amefanya poa na ngoma zake Wayu Wayu, Banana na Imani, alimkabidhi nyumba mama yake mzazi na kumtoa kwenye maisha ya kupanga huku akiweka wazi kuwa ilikuwa ni ndoto yake tangu baba yake mzazi afariki.