Friday , 2nd Oct , 2015

Mtayarishaji muziki ambaye pia ni mwimbaji, Jaco Beats ameamua kufikisha ujumbe wake wa amani na vilevile thamani ya kura kupitia rekodi maarufu ya 'Nerea' ya kundi maarufu la Sauti Sol, katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu mwisho wa mwezi.

Mtayarishaji muziki ambaye pia ni mwimbaji, Jaco Beats

Jaco Beats ameieleza eNewz kuwa, mahadhi ya rekodi hiyo ndiyo yaliyomsukuma kuitumia kutoa hamasa kutokana na kipindi ambacho Tanzania inapitia, akipata mapokezi mazito kutoka ndani na nje ya nchi ikiwepo vyama vya siasa ambavyo kwa kila pande vimeguswa na kazi hiyo.