
Alikiba ameyasema hayo katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio ambapo ameweka bayana kwamba tangu aanze muziki hakuwahi kuimba katika eneo la Mwembe Yanga Temeke Jijini Dar es salaam.
Alikiba ameyasema hayo aliposhiriki katika tamasha lililoandaliwa na East Africa Radio kwa nianba ya wana 17 ambalo lililenga kukutanisha mashabiki wa muziki jijini Dar es salaam na wasikilizaji wa EA Radio.
East Africa Radio imetimiza miaka 17 katika kuendesha kazi zake za kuelimisha, kuburudisha, na kuhabarisha katika ukanda wa Africa Mashariki.
Aidha katika kutimiza miaka hiyo kituo kimeweza kuendesha matamasha matano Coco Beach, Kigamboni, Gongo la Mboto, Tegeta Nyuki na Mwembe Yanga Temeke jijini jijini Dar es salaam.
